FAHAMU ATHARI ZA KUBEBA VYAKULA VYA MOTO KWENYE MIFUKO(RAMBO) AU VYOMBO VYA PLASTIKI

Maisha ya kila siku ya mwanadamu hususani katika nchi za kiafrika hutegemea kwa kiasi kikubwa matumizi ya vyombo vya plastiki kuhifadhia vitu mbalimbali kama vile vyakula ,mafuta  na maji. Imekuwa kama tamaduni watu kubeba vyakula kama vile chips,mihogo,maandazi ya moto kwenye mifuko ya rambo kama ijulikanavyo na watanzania wengi bila ya kutambua madhara yatokanayo na mifuko hiyo.

Tafiti zinaonesha kuwa plastiki ina madhara makubwa sana pindi ikikutana na joto kali ambapo hutoa kemikali iitwayo BPA(bisphonel A) ambayo ina madhara makubwa katika mifumo mbalimbali ya mwili wa binadamu .Nchi nyingi zilizoendelea zimepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kutokana na kutambua athari zake kwa jamii.

Kitaalamu plastiki imetengenezwa kwa kemikali zaidi ya mia mbili(200) ambazo huweza kusababisha zaidi ya aina hamsini(50) za saratani kwa mwandamu. Tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia sitini(60%) ya saratani zimesababishwa na matumizi ya vifaa vya plastiki.

Kutokana na ongezeko la matumizi ya plastiki nchini,ugonjwa wa saratani nao umeongezeka kwa kiasi kikubwa hususani kwa kina mama ambapo ugonjwa huu huleta mabadiliko kama vile

 • Mabadiliko katika mfumo wa uzazi
 • Mabadiliko ya kijenetiki
 • Matatizo katika mfumo wa homoni
 • Matatizo ya kushindwa kuona na
 • Matatizo katika uyeyushwaji waji wa chakula tumboni.

Watu wengi hutumia vifaa vya plastiki bila kujua madhara yake kwa sababu madhara hayatokei ndani ya siku moja bali ni baada ya miaka kadhaa kupita ndipo madhara kama saratani huanza kujidhirisha. Mfano watu wengi huchemsha maji na kuyahifadhi katika ndoo za plastiki yakiwa bado ni ya moto na baada ya muda ukichunguza ndoo ile utakuta mabaka mabaka yanayodhihirisha kuwa ndoo imeshatoa kemikali nyingi sana. Pia wanawake wengi hupenda kutumia mifuko aina ya Rambo kufunika vyakula kama vile wali kipindi wanapika ili kuivisha haraka bila kujua kemikali ambazo zinaingia kwenye chakula hicho zina madhara makubwa.

 

Bisphonel A(BPA) ni nini?

Hii ni kemikali ambayo inapatikana kwenye vifaa vingi vya plastiki tunavyotumia kila siku.Kiwango kikubwa cha kemikali hii kinahusishwa na ugumba na matatizo mengine ya kiafya. Vyanzo vingine vya kemikali hii  ni kama vilevifaa vya hospitali,midoli ya watoto,lenzi za miwani,vifaa vya kielektroniki vya majumbani pamoja na vifaa kadhaa vya michezo.

BPA ina tabia zinazofanana sana na homoni aina ya estrojeni hivyo basi kemikali hii huingilia mfumo wa uzalishaji,utunzwaji,usafirishwaji na kazi za homoni mbalimbali katika mwili.

Madhara yatokanayo na bisphonel A(BPA).

 • Magonjwa ya ini.
 • Magonjwa hatari ya moyo
 • Kisukari
 • Magonjwa ya kizazi kwa jinsia zote
 • Kuathiri nguvu za kiume
 • Kuathiri mfumo wa fahamu na kusababisha mtu kupoteza kumbukumbu
 • Pumu kuongezeka kwa wagonjwa wa pumu

Nini kifanyke?

1.Mtu binafsi kujiwekea mikakati ya kutokuweka vyakula vya moto kwenye mifuko ya plastiki.

2.Wauzaji wa vyakula kutumia mifuko maalumu iliyotengebezwa kwa ajili ya kuweka na kubeba vyakula vya moto.

3.Serikali kutekeleza sera za kupunguza matumizi ya vyombo na mifuko ya plastiki.

KUMBUKA

Madhara yatokanayo na matumizi ya plastiki huonekana baada ya muda mrefu kupita(long term effects)  hali ambayo husababisha watu wengi kuendelea kutumia vifaa vya plastiki bila kujali hadi pale madhara yatakapowapata na kushindwa kujua chanzo ni nini.

 

 

“Ijali afya yako na ya vizazi vijavyo kwa kupunguza matumizi ya vyombo vya plastiki.”

 

5 thoughts on “FAHAMU ATHARI ZA KUBEBA VYAKULA VYA MOTO KWENYE MIFUKO(RAMBO) AU VYOMBO VYA PLASTIKI

 1. Habari kaka,
  Naomba nikiri kuwa unafanya kazi nzuri sana, hii ni post ya kwanza kuisoma kwenye website yako kuna rafiki yangu kashare link. Kiukweli sijajutia muda wangu. Naahidi kufatilia kwa ukaribu post zako. Endelea kusambaza upendo. Mungu akuzidishie.

  1. Asanteh….. nashukuru sana pia kwa mda wako uliotumia kusoma ujumbe huu wa afya basi ni vizuri kuufanyia kazi na bila kusahau kuwakumbusha na wengine kupitia ulichojifunza kwani afya yako wewe ndio mtaji wako.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center