MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UJAUZITO ILI KUZUIA MAAMBUKIZO YA VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

Itawezekana kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto endapo mambo yafuatayo yatazingatiwa;

Matumizi sahihi ya ART kama ashauriwavyo na wataalamu wa afya. dawa hizi hupunguza idadi ya virusi hivyo huepusha maambukizi kwa mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.

Mama anapaswa kuzingatia usafi binafsi ili kuzuia maambukizo ya vimelea vya magonjwa. baadhi ya magonjwa huharibu plasenta hivyo kupelekea urahisi wa virusi kupita toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito

mama anapaswa kula mlo kamili na wenye lishe bora wakati wa ujauzito. itamuwezesha mama kuongeza kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi.
Mama anapaswa kuandaa mazingira salama ya kujifungua, hii ni pamoja na kuwahi kituo cha afya mara amapoona dalili za mwanzo za kujifungua. humwepusha mama kupata matatizo wakati wa kujifungua na pia mtoto atapata dawa za kujikinga na maambukizi mara tu baada ya kuzaliwa

Ni wakati upi mtoto yupo hatarini kupata maambukizo ya VVU kutoka kwa mama?

  •  wakati wa ujauzito, hasa mama anapopata maambukizo mapya kwani idadi ya virusi (viral load) huongezeka 
  • wakati wa kujifungua kama mtoto atapatwa na michubuko itakayo ruhusu virusi kutoka kwenye damu ya mama kupenya kwa mtoto 
  • wakati wa unyonyesha endapo mama atazidisha kumnyonyesha mtoto baada ya miezi sita au kumpa vyakula vingine kabla ya miezi sita.
wenza wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya pale wanapopanga kupata mtoto ili wapate ushauri sahihi wa jinsi ya kufanya kumkinga mtoto wao dhidi ya maambukizi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center