je, unafahamu maajabu ya kunawa mikono?

Pengine kunawa mikono ni jambo linaloonekana kuwa dogo na kupuuzwa na watu wengi, lakini kiuhalisia kutonawa mikono vizuri kama inavyotakiwa ni sababu kubwa ya kueneza magonjwa hatari sana yanayopelekea vifo kwa kiasi kikubwa. 

utangulizi

Mikono ni njia rahisi sana ya kusafirisha bakteria kutoka sehemu mbalimbali na kwenda mdomoni. Ni mara nyingi watu tumekua tukijiweka kwenye hatari kubwa sana ya kupata maambukizi ya magonjwa hatari yatokanayo na uchafu ambayo yanaweza kuhatarisha maisha kama vile kipindupindu, homa ya matumbo na kuhara. Mikono ina uwezo wa kubeba bakteria wengi sana wa aina mbalimbali kutoka kila sehemu unazogusa. Kwa mfano hebu fikiria unapopanda basi, unajua aliyeshika lile bomba alishika nini kabla? Hivyo ni lazima kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na sabuni kila mara hasa kabla ya kula na baada ya kutoka chooni.

 

Kunawa mikono ni nini?

Kunawa mikono ni kitendo cha kusafisha mikono kwa maji safi yanayotiririka pamoja na sabuni  kwa nia ya kuondoa vumbi, uchafu na vijidudu mbalimbali vya magonjwa. Ni muhimu kufahamu kuwa endapo  sabuni haipatikani, unaweza kutumia jivu au mchanga kama mbadala. Kumbuka kuwa hata kama mikono yako inaonekana misafi, inaweza kuwa na vijidudu vya magonjwa au mayai ya minyoo hivyo kusababisha madhara vitakapoingia mwilini endapo utakula bila kunawa vizuri.

Ni wakati gani napaswa kunawa mikono?

 • Wakati wa kuandaa chakula
 • Kabla na baada ya kula.
 • Kabla na baada ya kumhudumia mgonjwa
 • Kabla na baada ya kusafisha kidonda.
 • Baada ya kutoka chooni.
 • Baada ya kumsafisha mtoto aliyetoka kujisaidia
 • Baada ya kushika mifugo au kusafisha mabanda yao
 • Baada ya kukohoa au kupiga chafya.

Jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi…..

Kunawa mikono ni kitendo rahisi na cha haraka ingawaje kinatakiwa kifanywe kwa usahihi ili kuweka mikono safi na kuzuia kueneza magonjwa ambayo ni hatari kwa afya zetu. Unaponawa nikono yako zingatia hatua zifuatazo-;

 • Lowanisha mikono yako kwa kuinyunyizia maji
 • Paka sabuni kwenye viganja vya mikono kutengeneza povu
 • Sugua mikono vizuri sehemu zote kuanzia vidole, katikati ya vidole na kuzunguka kucha za vidole pia
 • Mimina maji safi juu ya mikono yako na suuza vizuri
 • Kausha mikono yako kwa kitambaa safi

 

Acha kunawa mikono kwa mazoea...

Ni mara nyingi watu wengi hunawa mikono bila kuzingatia taratibu na kanuni zinazotakiwa. Ni jambo la msingi sana kunawa mikono vizuri kuhakikisha inakuwa safi mda wote ili kuepukana na magonjwa. 

hakikisha watoto wananawa mikono wanapotoka kucheza

jijengee desturi ya kunawa mikono kila wakati

unaweza kutumia kibuyu chirizi kama hakuna bomba nyumbani

nawa mikono yako kila baada ya kutoka chooni na kabla ya kula

.......karibu tena daktari mkononi ujifunze mengi zaidi...

12 Comments

 1. Thank you very much doctors for this education it so helpful for the people who are not aware of this issue and also reduces the transmission of diseases and finally people will be safe from the transmitted diseases……Thank you and be blessed always🙏🏻

 2. Hongera sana kwa kuliona hili maana imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya maeneo hasa vijijini ambako kipindupindu na matumbo ya kuhara yameathiri kwa kiasi kikubwa.Hivyo ni vizuri elimu hii pia watu wa vijijini wakaipata,Asante

 3. mmekumbusha jambo muhimu kwa ustaw wa afya zetu.ila elimu itolewa pia kwa wauzaji vyakula hasahasa mitaani kutumia maji safi ,na salama kwa kunawa na pia mashuleni

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.