JE NAWEZA KUPATA MADHARA NAPOVUTA MOSHI WA SIGARA HATA KAMA MIMI SIVUTI?

Utafiti unaonyesha kwamba uvutaji wa pili wa sigara kitaalamu kama second hand au passive smoking huleta madhara ya kiafya  kwani ni mchanganyiko wa moshi unaotoka mdomoni mwa mvutaji kitaalamu kama mainstream smoke na moshi unaotoka kwenye sehemu ya mwisho ya sigara kitaalamu kuitwa sidestream smoke.

Madhara ya muda mrefu yatokanayo na uvutaji wa pili ;

  • Magonjwa ya mapafu

asilimia 20 hadi 30 ya watu wasiovuta sigara wakikaa katika mazingara ya watu wanaovuta sigara huweza kupata kansa ya mapafu

  • Kujihatarisha na magonjwa ya moyo

Uvutaji wa pili wa muda mrefu husababisha damu iliyo kwenye mzunguko kuganda na kutengeneza mabonge bonge yanayoweza kukuhatarisha na magonjwa ya moyo

  • Lakini pia uvutaji wa pili hupunguza kiwango cha kemikali zinazokukinga na magonjwa mbalimbali katika mwili wako
  • Kwa mama mjamzito husababisha kujifungua kabla ya muda                                                                            

Nini cha kufanya?

  • Kama wewe ni mvutaji wa sigara kumbuka kwamba moshi wa sigara husambaa kwa haraka sana kwa njia ya hewa na hivyo mtu yeyote anaweza akauvuta na akapata madhara ya kiafya,hivyo basi ni vema unapovuta sigara usogee mbali kidogo na watu wengine ili kuepusha madhara hayo
  • Kwa ambaye sio mvutaji epuka mazingira ambayo watu wanavuta sigara
  • Kama ni katika kichumba kidogo basi fungua dirisha kuruhusu hewa itoke ili usipate madhara makubwa

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center