Mama mjamzito kutokwa na jasho sana tatizo ni nini?

Kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho huambatana sana na mabadiliko mbalimbali ya mwili ya mwanamke. Baadhi ya mabadiliko hayo ni pamoja na kubadilika mara kwa mara kwa mihemuko (mood swing), kuchoka haraka, kutokwa jasho sana.

Wanawake wengi katika kipindi cha ujauzito hutokwa sana na jasho hasa wakati wa usiku.

Je nini husababisha?

Mabadiliko ya viwango vya vichochezi vya mwili (homornes); kipindi cha ujauzito huambatana na mabadiliko ya viwango vya vichochezi, mabadiliko haya huuweka mwili katika hali ya kuweza kubeba ujauzito kwa kipindi cha miezi yote 9.

Kichochezi aina ya projesteroni huongezeka na kuwa katika kiwango kikubwa katika damu wakati wa ujauzito, mabadiliko haya hupelekea mishipa mingi ya damu iliyo karibu na ngozi kutanuka hivyo kuruhusu damu kupita kwa wingi hivyo kuongeza kiasi cha maji yanayopotea kwa njia ya jasho.

Kutokwa na jasho husaidia kuupoza mwili hivyo hii hutokea ili kuuweka mwili katika hali ya msawazo wa joto.

Kufanya kazi nzito: Mama mjamzito kwa kawaida huchoka haraka hata baada ya shughuli ndogo. Hivyo iwapo mama mjamzito anafanya shughuli nzito huweza kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha jasho kinachotolewa.

Maambukizi ya magonjwa: Wakati mwingine kutokwa na jasho sana hasa wakati wa usiku huweza kuwa ni dalili ya mwanzo ya homa (fever) ambayo huashiria kuwepo kwa maambukizi ya magonjwa. Hivyo ni vyema kama ukiona hali ya kutokwa na jasho si ya kawaida, basi wahi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

Je nifanye nini kupunguza kutokwa na jasho sana?

  • Pendelea kukaa maeneo ya wazi ambako kuna mzunguko mkubwa wa hewa safi.
  • Pia epuka kuvaa nguo nyingi au zinazobana mwili bali pendelea kuvaa nguo nyepesi kwani huruhusu mzunguko wa hewa.
  • Pendelea kufanya mazoezi mepesi
  • Ni vyema kuoga kabla ya kulala

Kwa sababu kutokwa na jasho kwa wingi husababisha mwili kupoteza maji sana hivyo basi ni vyema kunywa maji ya kutosha kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center