Ni muda upi sahihi wa kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI?

Utangulizi……

Kuna njia nyingi ambazo mtu huweza kupatwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi mfano kupitia ngono isiyo salama, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kuongezewa damu isiyo salama au kuchangia vifaa vyenye ncha kali. Inatakiwa kujijengea desturi ya kupima mara kwa mara ili kupata uhakika wa hali ya afya uliyonayo na uweze kuanza matibabu mapema iwezekanavyo kabla kinga ya mwili haijashuka na kupelekea magonjwa nyemelezi.


Ni mara ngapi natakiwa kupima virusi vya UKIMWI?

Watu wote hasa walio kwenye umri wa kuzaa (sexually active)  wanatakiwa kupima maabukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa kama vile kaswende na kisonono. Kadiri unavyokuwa na wenza wengi, ndivyo unavyotakiwa kupima magonjwa ya zinaa. Hii ni kwasababu baadhi ya magonjwa ya zinaa huchelewa kuonesha dalili.


soma zaidi

Ni muda gani sahihi wa kupima baada ya kuhisi nimeambukizwa virusi vya UKIMWI?

Kama unahisi umepata maambukizi ya virusi vya ukimwi aidha kutokana na kufanya ngono isiyo salama au njia nyingine zinazoweza kupelekea maambukizi unatakiwa ukapime haraka iwezekanavyo ili kupata kinga inayotolewa baada ya maambukizi (post exposure prophylaxis) ambayo husaidia usipate maambukizi. Kwa kawaida muda unaochukua kutoka maambukizi mpaka kipimo kuonesha majibu chanya ni baada ya wiki mbili mpaka miezi mitatu kutegemea na kinga ya mtu na kipimo kilichotumika.


soma zaidi

Nini faida ya kupima mara kwa mara?

Watu wengi wamekuwa na dhana ya kuogopa kupima maambukizi ya virusi vya ukimwa kwa kuhofia msongo wa mawazo endapo wakipatikana na maambukizi.  Wengi hupenda kusema “Nipime natafuta nini”?  Inakupasa ufahamu kwamba unapopima na kujua hali yako inakusaidia wewe mwenyewe kujikinga na maambukizi vilevile inasaidia kutosambaza kwa watu wengine.

“Kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI inawezekana”, pima afya yako sasa!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center