Ninapaswa kufahamu nini kuhusu Tiba Ya Homoni ? (Hormonal Therapy)

Tiba ya homoni ni uongezaji wa homoni zinazokosekana mwili hasa kwa wanawake waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause). Hii ni kutokana na athari wanazopata wanawake kutokana na kukosekana kwa homoni hizi kama vile kulainika kwa mifupa (osteoporosis) au tatizo la kutibuka joto (hot flashes).

Tiba hii ya homoni huhusisha matumizi ya:

 • Vidonge vya estrojeni:

Hii ndio njia iliyozoeleka zaidi. Estrojeni ni homoni ya kike ambayo hupungua sana wakati wa kukoma kwa hedhi. Fuata maelekezo ya daktari katika kutumia dawa hizi kwani homoni hizi hufuata mzunguko maalumu.

 • Kipandikizi cha estrojeni:

Hii hupandikizwa chini ya ngozi ya tumbo. Kisha hubadilishwa baada ya siku kadhaa au wiki.

 • Estrojeni ya kupaka:

Hii hupakwa kwenye ngozi na kisha hupenya hadi kwenye damu na kusambazwa mwili mzima. Baadhi hupakwa kwenye ngozi ya mkono mmoja kutoka kwenye uvungu wa kiganja hadi kwenye bega na nyingine hupakwa kwenye mguu kutegemea maelekezo ya dawa husika na hupakwa kila siku.

 • Vidonge vya projestini:

Hii ni homoni nyingine ya kike (mbadala wa projesteroni) ya kutengeneza lakini huweza kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya mji wa mimba.

 • Tiba mchanganyiko:

Hapa homoni ya estrojeni na projestini huchanganywa ili kuleta manufaa zaidi.

Kwa upande mwingine, Tiba hii huweza kuleta hali zisizo za kuvutia mwilini kama vile:

 • Uvimbe katika matiti
 • Maumivu ya kichwa
 • Kisirani (Mood Changes)
 • Kichefuchefu
 • Kutoka damu ukeni

Je, ni nani hashauriwi kutumia tiba ya homoni ?

 • Mwenye matatizo ya kuganda kwa damu (Blood clots)
 • Mwenye Kansa ya Matiti au mji wa mimba.
 • Mwenye magonjwa ya Ini au moyo
 • Wajawazito
 • Mwenye mshtuko wa moyo

Ni muhimu pia kufahamu kuwa tiba hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu hivyo ni muhimu kupata ushauri wa daktari au mtaalamu ili kujua ni dawa gani itafaa zaidi kwako na kwa dalili ulizo nazo.

1 thought on “Ninapaswa kufahamu nini kuhusu Tiba Ya Homoni ? (Hormonal Therapy)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center