KWANINI MWANANGU HASHIBI?

Utangulizi

Maziwa ya mama kwa mtoto ni jambo la muhimu sana kwani yana virutubisho vingi vinavyomsaidia mtoto kukua vizuri, kumkinga na magonjwa na kumsaidia kupona haraka anapoumwa. ndio maana inashauriwa mtoto kunyonya maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza, na baada ya hapo kuanzishiwa vyakula vya kawaida pamoja na kunyonya mpaka anapofikisha miaka miwili. watoto wengi wanaugua kwasababu ya kukosa virutubisho vya muhimu mwilini na hii hutokana na kutokunyonya maziwa ya kutosha.

SABABU

Mama kumbeba mtoto vibaya wakati wa kumnyonyesha, inashauriwa mama kushiriki kimwili na kiakili katika kumnyonyesha mtoto hasa kwa kumwangalia mtoto ili kujua kama maziwa yameisha, kapaliwa, chuchu imetoka mdomoni n.k. pia inashauriwa kumuacha mtoto anyonye ziwa moja kwa takribani dakika 10-15 kabla hujamuhamisha ziwa jingine na ukaendelea hivo adi ashibe.

 Kuchelewa kumnyonyesha mtoto, inashauriwa kumnyonyesha mtoto mara nyingi iwezekanavyo na sio kusubiri alie, au akiamka. Hii itamsaidia mtoto kuwa na chakula mwilini mwake kila wakati hivyo kumfanya mwenye afya na ukuaji bora. Yafaa sana kutompangia mtoto muda wa kunyonya na pia kuhakikisha ananyonya hata wakati wa usiku.

Hakikisha mtoto anapata muda mrefu wa kunyonya, hii pia humsaidia mtoto kumtambua mama ake na kujenga ukaribu wa hali ya juu nae. pia ni muda mzuri wa kuongea na mtoto na kumuonesha furaha.

matumizi ya chupa, pacifier, vyakula na vimiminika vyovyote kwa watoto wenye umri chini ya miezi sita si mazuri kabisa. kwani hizi ni njia rahisi sana za kumletea magonjwa mtoto kutokana na uchafu. watoto wengi wanaotumia vitu hivi hushambuliwa na magonjwa ya kuhara. hivyo basi ni vema kumnyonyesha mtoto ili kumkinga na magonjwa yaletwayo na uchafu.

hali ya mama kisaikolojia mfano woga, mawazo, sonona, kutopenda kunyonyesha,kuchoka na kumkataa mtoto, haya yote huchangia mtoto kukosa maziwa ya kutosha au hata kukosa maziwa kabisa. inashauriwa mama kutambua hali hiyo mapema na kujitahidi kukabiliana nayo kama inawezekana. lakini ikishindikana yafaa basi kuonana na daktari kwa ajili ya kumsaidia.

hali ya mama kiujumla, mfano magonjwa sugu kama kifua kikuu, upungufu wa damu, mama kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, kuwa na mjamzito, kuvuta sigara, kunywa pombe, haya yote huathiri utengenezaji wa maziwa pia humfanya mama kua mchovu hivyo kushindwa kumnyonyesha mtoto vizuri na kwa mda mrefu hadi kushiba.

hali ya mtoto kiujumla mfano ugonjwa ambao unamfanya asinyonye vizuri kama mdomo sungura, magonjwa ya moyo, utambuzi wa magonjwa haya mapema yatasaidia katika matibabu ya haraka.

Ikumbukukwe ya kuwa, Mama kuwa na ukimwi si kigezo cha kutomnyonyesha mtoto.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center