Nawezaje kupika mboga za majani bila kupoteza virutubisho vyake?

Mboga za majani ni aina ya chakula ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha na kujenga miili yetu

Lakini je , upikaji wetu ni sahihi ?

Zifuatazo ni njia mbalimbali zinazosaidia katika utunzaji na namna ya kuzipika ili kuweza kutunza na kupata virutubisho vyake muhimu katika kujenga miili yetu.

UTUNZAJI WAKE

Nunua mboga mboga na matunda kadiri ya uhitaji wako na uzipike hapo hapo au ndani ya siku mbili ,Utunzaji wa muda mrefu wa mboga za majani hupoteza virutubisho vingi vilivyomo na vyenye umuhimu ndani yake,epuka kuzinunua kwa wingi na kuishia kuzitunza kwa muda mrefu.

Inapotokea umenunua mboga mboga na matunda mengi, basi weka kwenye jokofu la barafu lenye nyuzi 4 au chini ya hapo ili kuweza kutunza virutubisho vyake vya muhimu.

Vile vile pendelea kutunza vyakula kwenye sehemu ya giza na ubaridi kwani vyakula vingi hupoteza virutubisho vyake vinapokaa kwenye sehemu za  mwanga na joto.

UANDAAJI WAKE

Osha mboga mboga na matunda yako kwa maji yanayotiririka kama  kwenye bomba  ili kuweza kutoa vijidudu vinavyoweza kuleta madhara kwenye afya zetu,hivyo epuka kuziloweka kwenye chombo kwani baadhi ya vitamini hupotea kwa njia ya maji.

Pia epuka kumenya maganda ya mboga mboga na hata matunda kwani maganda yake ndiyo yenye virutubisho vingi kuliko hata tunda lenyewe

NAMNA YA KUPIKA

Chagua njia ambazo zitatunza virutubisho vilivyomo kwenye mboga mboga zako ambazo hazitumii moto mwingi utakao ua na kupoteza virutubisho vya muhimu. Hivyo tumia njia ya kupika kama  kwa kutumia mvuke kwani hutumia moto kidogo na hata rangi ya mboga haibadiliki na hukufanya kuweza kupata  na kutunza virutubisho vyote

Vile vile ni vizuri uzipike bila kukata kata , kwani unapokata unazidi kuongeza uwezekano wa kupoteza virutubisho muhimu.

Pasha moto mboga zako pale ambapo unauhitaji tu, epuka kupasha mara kwa mara  ili kuweza kutunza virutubisho vilivyomo kwenye mboga zako.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center