Fahamu jinsi unywaji wa pombe unaweza kumuathiri mwanamke zaidi ya mwanaume?

Miili ya wanawake inaathirika  na vilevi tofauti na miili ya wanaume ,hivyo kupelekea wanawake kupata  madhara zaidi  kuliko  wanaume.

Inasemekana kwamba hata kama mwanamke akiwa na uzito sawa na mwanaume na wakatumia vilevi sawa kwa muda mmoja mwanamke atawahi kuudhurika kuliko mwanaume.

Hii ni kwasababu mwanamke na mwanaume wana miili tofauti na pombe humengenywa tofauti vile vile.

Mwili wa mwanamke una kiwango cha  maji kidogo na mafuta mengi tofauti na mwili wa mwanaume wenye kiwango cha maji mengi na mafuta kidogo ,maji huyeyusha pombe mwilini na mafuta huitunza.Hivyobasi mwili wa  mwanaume utaweza kuyeyusha pombe kwa kiasi kikubwa na kuitunza kidogo kuliko mwili wa mwanamke.

Vilevile mwili wa mwanamke huwa na kiwango kidogo cha kimengenya cha kilevi  kitaalamu huitwa alcohol dehydrogenase ,kinachosaidia kumengenya kilevi kabla haijafika kwenye damu.

Kumbuka unywaji wa kiasi ni silaha kwa afya bora.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.