MAGONJWA YAENEZWAYO NA MAJI MACHAFU (HOMA YA MATUMBO)

HOMA YA MATUMBO

Homa ya matumbo ama typhoid fever kwa kingereza, ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella typhi anayeenezwa kwa njia ya maji au chakula chenye kinyesi au chembechembe za kinyesi cha mtu aliyeambukizwa

DALILI

Homa kali

Kutoka kwa jasho sana

Kuharisha bila kutoka damu

Je bila matibabu nini kitatokea!?

Kama mgonjwa hajapata matibabu , homa ya matumbo hugawanyika katika hatua 4 , wiki moja kwa kila hatua

• Joto la mwili huongezeka
• Kichwa huuma
• Kukohoa
• Maumivu ya tumbo

• Kuongezeka kwa homa
• Mgonjwa huanza kuchanganikiwa
• Kutapika
• Vitone vyekundu hutokea kifuani
• kuvimba ini

• matumbo hutoboka na kutoa damu
Hatua ya tatu ikimalizika , homa huanza kutulia, hii huendelea hadi hatua ya nne

MATIBABU

Dawa kama ampicillin,chloramphenicol trimethoprim,sulfamethoxazole,amoxicillin husaidia kutibu homa hii

NAMNA YA KUEPUKA KUPATA HOMA HII

 
• kunywa maji yaliyo safi na salama ama chemsha maji kwa ajili ya kunywa
• nawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni na kabla ya kula
• osha matunda na mbogamboga vizuri kabla ya kula au kupika
• kula chakula kilichoiva vizuri na kisiwe kimepoa sana

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center