MAGONJWA YAENEZWAYO KWA MAJI (KIPINDUPINDU).

UTANGULIZI

Kipindupindu ama cholera  kwa kingereza ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria anayeitwa Vibrio cholera hasa kwenye utumbo mwembamba.  Maambukizi hutokea hasa kupitia maji au vyakula vilivyochafuliwa na wadudu kama vile nzi.

MAAMBUKIZI

Endapo  maji ya chooni hasa yenye kinyesi yakichanganyikana na maji yanayotumika kwa kunywa , watu hupata bakteria hao, vilevile bakteria hawa hupatikana katika maji ya bahari, mto au ziwa yaliyochafuliwa na kinyesi.Samaki na vyakula vingine kutoka kwenye maji yaliochafuliwa husababisha maambukizi pia.

 • Kuharisha majimaji yenye rangi ya maji ya mchele
 • Kutapika
 • Tumbo kuuma sana
 • Kukosa nguvu
 • Mgonjwa hupatiwa maji mengi kwani hupoteza maji mengi kwa kutapika na kuharisha
 • Dawa kama cotrimoxazole,erythromycin,doxycycline,chloramphenicol,furazolidone husaidia.
 • Katika baadhi ya nchi, chanjo hutolewa
 • Tumia maji yaliyotibiwa ama chemsha maji kwa ajili ya kunywa
 • Tumia choo kwa kila haja, usiende haja au kutupa kinyesi katika vyanzo vya maji
 • Nawa mikono kwa sabuni na maji masafi yanayotiririka hasa ukitoka chooni na kabla ya kula
 • Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa ya klorini ili kuua bakteria
 • Osha na umenye matunda kabla ya kula na usile majani ya matunda
 • Pika chakula vzuri na katika hali ya usafi
 • Nawa mikono vzuri kabla ya kutayarisha chakula

Funika chakula na maji ikiwa hauli

1 thought on “MAGONJWA YAENEZWAYO KWA MAJI (KIPINDUPINDU).

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center