MAGONJWA YAENEZWAYO KWA MAJI (KUHARA).

UTANGULIZI!

Ugonjwa wa kuhara unajulikana pia kwa jina la umwagaji hatari wa damu ama dysentery kwa kingereza unatokana na machafuko ya maini na hasa matumbo yanayosababisha kuharisha ambapo kuna damu na/au kamasi katika kinyesi

SABABU!

Ugonjwa  husababishwa na bakteria kama Shigella na Campylobacter, protozoa kama amoeba,  vimelea ama minyoo lakini pia baadhi ya kemikali au virusi ambao huambukizwa kwa njia ya kula chakula,matunda ama kunywa maji na vinywaji vilivyo na vilivyochfuliwa na visababishi hivi

 

 • Kuhara
 • Kutapika damu
 • Kuwepo kwa damu au /na kamasi (inategemea na aina ya vmelea vlivyosababisha)
 • Tiba ya maji (maji huchanganywa na chumvi na sukari), mgonjwa anapaswa kuwekewa maji mwilini ili kuhakikisha kiwango cha maji mwilini kipo sawa
 • Kama imebainikia kuwa ugonjwa umesababishwa na Shigella dawa kama ciprofloxacin au TMP-SMX(Bactrim) husaidia. Lakini Shigella imekuwa sugu hivyo matibabu ya kina hutakiwa
 • Kama ugonjwa umesababishwa na Amoeba dawa kama metronidazole (flagyl), paromomycin (humatin), iodoquinol (yodoxin)
 • Tembe za Zinki
 • Tumia maji yaliyotibiwa ama chemsha maji kwa ajili ya kunywa
 • Tumia choo kwa kila haja, usiende haja au kutupa kinyesi katika vyanzo vya maji
 • Nawa mikono kwa sabuni na maji masafi yanayotiririka hasa ukitoka chooni na kabla ya kula
 • Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa ya klorini ili kuua bakteria
 • Osha na umenye matunda kabla ya kula na usile majani ya matunda
 • Pika chakula vzuri na katika hali ya usafi
 • Nawa mikono vzuri kabla ya kutayarisha chakula
 • Funika chakula na maji ikiwa hauli
 • Hakikisha unamlisha mtoto chakula kisafi na salama

1 thought on “MAGONJWA YAENEZWAYO KWA MAJI (KUHARA).

 1. Shukran Sana Dr kwani niimani yangu kwamba kwahaya machache uliyotusaidia kuyachambua tukiyazingatia tutakua salama sisi pamojaa nafamilia zetuu siku zote..
  Ahsanteni sanaa

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center