Wanawake hatarini kupata maambukizi ya njia ya mkojo. Sababu ni nini?

fahamu njia ya mkojo…

Njia ya mkojo kama inavyoitwa kitaalamu (urinary tract) ni mfumo wa mwili unaohusiana na kutoa kimiminika kisichohitajika kutoka katika mwili wa binadamu kwa njia ya mkojo. Mfumo huu unahusisha figo, ambazo huchuja uchafu kutoka katika kimiminika hicho ili kutengeneza mkojo, kibofu cha mkojo ambacho huhifadhi mkojo kwa muda mfupi kabla haujatolewa, mirija ya ureta ambayo husafirisha mkojo kutoka katika figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo pamoja na mrija wa urethra ambao hutoa mkojo nje ya mwili. 

Fahamu kuhusu UTI…

UTI ni kifupisho cha Urinary Tract Infections. Ni maradhi yanayosumbua watu wengi ikiwemo watoto, vijana na watu wazima. Hushambulia sehemu za mfumo wa mkojo kama zilivyotajwa hapo juu. Kwa kifupi UTI hushambulia viungo vinavyohusika katika kupitisha mkojo kabla haujatoka nje ya mwili.


Soma zaidi

UTI husababishwa na nini?

UTI husababiswa haswa na bakteria anayejulikana kwa jina la Escherichia coli ambaye hupatikana kwenye utumbo mkubwa na njia ya haja kubwa. Lakini hatari ni pale bakteria huyu anapoingia kwenye mfumo wa mkojo ampapo huzaliana na kusababisha maambukizi.

kwanini UTI inawaathiri sana wanawake?

Kama inavyojulikana tatizo hili la maambukizi ya njia ya mkojo huwapata wote wanaume kwa wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kwa sababu ya maumbile yao; yaani mrija ambao hutoa mkojo kutoka kwenye kibofu kwenda nje ya mwili(urethra) ni mfupi zaidi, hivyo basi ni rahisi zaidi kwa vijidudu vya bakteria kutoka kwenye uke kupita kwenye mrija huo na kwenda kuleta maambukizi ya UTI kwenye mfumo wao wa mkojo.

inaendelea…

  • Ukaribu uliopo kati ya uwazi wa kupitisha mkojo na wa kupitisha haja kubwa.               Hii hupelekea urahisi wa bakteria wasababishao UTI kupita kutoka haja kubwa kwenda kwenye mfumo wa mkojo
  • Ukaribu kati ya mrija wa urethra na vagina. Hapa panahusisha tendo la ndoa ambapo bakteria hawa wanaweza kutoka kwa mwanamume wakati wa kujamiiana na kuweza kuingia kwenye njia ya mkojo kupitia urethra hivyo kuleta UTI.
  • Njia ya asili ya wanawake katika kutoa haja ndogo.Kama ilivyozoeleka kwamba, wanawake hujisaidia haja ndogo wakiwa wamechutama hali ya kuwa wanaume husimama hivyo ni rahisi kurudi kwa chembechembe za uchafu kama haja kubwa katika mfumo wa mkojo wa mwanamke hususani kama choo kinachotumika hakina usafi stahiki.

mambo unayoweza kufanya kujikinga na UTI…

Kuna hatua unazoweza kuchukua ili usipatwe na maambukizi ya ugonjwa huu kirahisi. Hii ni pamoja na kujifuta au kutawadha ukianzia mbele kwenda nyuma baada ya haja kubwa au ndogo. Kunywa maji mengi kila siku. Haifai kuubana mkojo kwa muda mrefu, timiza haja mara itokeapo. Pia jenga utaratibu wa kusafisha sehemu za siri mara kwa mara.

dalili za uti….

Habari njema ni kwamba licha ya wanawake kuwa wahanga wakubwa wa UTI kwa asilimia 30 kuliko wanaume , UTI inaweza kuepukika pia kutibika na tiba hii inabidi ifanyike haraka kabla maambukizi hayajafika ndani zaidi katika viungo vya mwili kama vile figo, kwani inaweza kusababisha figo kufeli kabisa kama isipotafutiwa ufumbuzi mapema. Hivyo basi, wahi kituo cha afya kwa uchunguzi na matibabu mara utakapojisikia dalili zifuatazo:-

hamu ya kukojoa mara kwa mara.

Maumivu ya kiuno pamoja na mgongo.

maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

kutoka damu kwenye mkojo.

Asante kwa kujifunza nasi……usikose kutembelea tena tovuti yetu ya daktari mkononi kufahamu muendelezo wa makala hii itakayohusu UTI kwa wanaume na mambo mengine mengi.

soma na weka maoni yako hapo chini.

2 thoughts on “Wanawake hatarini kupata maambukizi ya njia ya mkojo. Sababu ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show