MASWALI, MAJIBU NA MAONI.

Jacquilline kutoka Arusha: kuna muda jicho langu la kushoto huona nusu, shida ni nini?

Jibu: kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha tatizo hilo. Yawezekana ni tatizo kwenye mfumo wa macho au pia tatizo katika mfumo wa ubongo au kuumwa kichwa sana nk. Inashauriwa kumuona daktari au kituo cha huduma ya macho haraka iwezekanavyo.

Thereza kutoka Misungwi: kwanini macho yangu yanatoa machozi na kuwasha sana?

Jibu: macho kuwasha hutokana namambo kadhaa kama:

  • Kupata aleji au kuvimba (inflammation).

  • Kope kugusana na jicho au kitu kuingia jichoni.

  • Macho kuwa makavu (kutokua na machozi ya kutosha).

  • Kutumia vitu vinavyoweza kuleta muwasho kwenye macho kama manukato nk.

  • Matumizi ya lenzi za kuweka ndani ya macho (contact lens) nk.

Anisia kutoka Singida: je, kuna tatizo lolote linaloweza kutokana na kukuna macho endapo yatawasha?

Jibu: kukuna macho yanayowasha huweza kusababisha madhara zaidi kwenye jicho, huweza kusababisha jicho kuuma na kuvimba (inflammation) na kuharibu mboni ya jicho. Pia mikono yetu ina vimelea vingi, kukuna jicho hupelekea vimelea hivo kuingia jichoni na kuleta madhara mengine.

Anisia kutoka Kilimanjaro: njia mbadala ya kutatua tatizo la macho kuwasha baadala ya kuutumia dawa ni ipi?

Jibu: safisha macho yako na maji mengi, baridi na masafi au safisha na kitambaa kisafi cha maji ya baridi.

User 1 kutoka Dar: uchafu ukiingia jichoni hutolewaje?

Jibu: uchafu hutolewa kwa njia ya machozi, endapo ukiingia jichoni, mwili huutoa kwa kutoa machozi na kusafisha macho.

 

 

 

Privacy Preference Center