Muendelezo wa nakala ya kwanza kuhusu

Miguu yangu inachanika (Magaga) chanzo ni nini?? Part 1

 • Loweka miguu iliyopasuka kwenye maji ya uvuguvugu yenye sabuni kwa muda wa dakika 15 hadi 20.
 • Kisha loweka miguu kwenye maji kiasi cha galoni moja kwa muda wa dakika 10, maji hayo yachanganywe na kikombe kimoja cha asali. Kufanya hivi husaidia kuondoa Ngozi iliokufa pamoja na kuzuia damu kutoka katika mipasuko hio.

 • Sugua miguu kwa jiwe laini maalumu kwa kusugulia miguu na lisilo kwangua sana.

         

 • Kausha miguu vizuri kwa taulo au kitambaa cha pamba hasa kati kati ya vidole vya miguuni ili kuzuia kuvu(fangasi) na bakteria kuzaliana kwa urahisi miguuni.
 • Paka mafuta, cream ya miguu au lotion yenye virutubisho vya vitamini E, siagi au Aloevera. Mafuta ya nazi au parachichi pia yanaweza kutumiwa kulainisha miguu. Vipodozi hivi vitumike mara mbili asubuhi na jioni kila siku.

 • Vaa soksi kila siku unapokwenda kulala wakati wa usiku, kuvaa soksi nyeupe husaidia kuzuia vumbi lisingie ndani ya mipasuko ya miguu. Soksi nyeupe ni nzuri kwa vile hazitunzi joto jingi na kusababisha unyevunyevu miguuni, pia kuimarisha usafi kwan uchafu huonekana haraka kwa weupe wake.

 • Dhibiti magonjwa au hali zinazochangia kupasuka miguu, kama vile Ngozi kavu (kitaalamu inaitwa Xerosis).
 • Dhibiti uzito mkubwa kupita kiasi.
 • Dhibiti kisukari.

 

Mambo ya kutokufanya ukiwa na mipasuko ya miguu(Magaga)

 1. Usitumie wembe au kisu kukata/kuondoa mipasuko.
 2. Usitumie miti/kijiti kusugua kati kati ya mipasuko endapo itawasha.

 

Kuna madhara gani miguu ikipasuka?

 1. Urahisi wa vimelea vya bakteria au kuvu kuzaliana kati kati ya mipasuko mguuni.
 2. Kutokwa na damu pasipo kujua.
 3. Kufa ganzi maeneo karibu na mipasuko.
 4. Kuharibu muonekano wa mtu binafsi uzuri unapungua kwa kiasi.
 5. Muda mwingine hupata maumivu ya miguuni.

Privacy Preference Center