ATHARI NA MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA ARVs

ATHARI NA MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA ARVs

ATHARI, MATUKIO HATARISHI NA SUMU ZINAZOHUSIWA NA DAWA ZA VVU / UKIMWI

Dawa za VVU / UKIMWI (aina zote) zinazotumika kutibu watu wazima, vijana, watoto na wanawake wajawazito / mama wanaonyonyesha zinajumuisha mchanganyiko wa dawa kama vile TLD (Tenofovir, Lamivudine, na Dolutegravir), TLE (Tenofovir, Lamivudine, Efavirenz), ALD (Abacavir, Lamivudine, Dolutegravir), na dawa kama Zidovudine (AZT), Atazanavir (ATV), Lopinavir (LPV), Emtricitabine (FTC), Darunavir (DRV), na Raltegravir (RAL). 

Dawa hizi zinahusishwa na athari na madhara tofauti kulingana na muundo wa dawa ambayo inaelezewa kama ifuatavyo kwa kila dawa

  • Tenofovir (TDF) ina madhara kama figo kufeli, udhaifu wa mifupa na kuharibu ini.
  • Lamivudine (3TC) ina athari kama maumivu ya kichwa, kupungua uzito wa mwili, kichefuchefu
  • Dolutegravir (DTG) hii inahusishwa na madhara kama kuongezeka kwa mafuta mwilini, uharibifu wa figo na hutolewa kwa tahadhari kwa watu wenye shinikizo la damu na wenye kisukari
  • Abacavir (ABC) hii atahri zake mwilini ni kuumwa kichwa kuhara na kukosa hamu ya kula huku hutolewa kwa tahadhari kwa watu wenye magonjwa ya ini na kwa wamama wanaonyonyeshwa
  • Zidovudine (AZT) hii huleta madhara kama upungufu wa damu, maumivu ya misuli na kuharibika kwa ini na hutolewa kwa tahadhari kwa wenye ukosefu wa damu na wenye CD4 chini ya 200
  • Efavirenz (EFV) athari za dawa hii ni kama kushindwa kulala, kuota ndoto mbaya usiku, kuwa na wasiwasi, sonona na hutolewa kwa tahadahri kwa wagonjwa wa akili na wenye matatizo ya degedege.

  • Nevirapine (NVP) athari zake ni kama kuharibu ini na hutolewa kwa tahadhari kwa wenye CD4 zaidi ya 400 kwa wanaume na CD4 zaidi ya 250 kwa wanawake na wenye magonjwa ya ini

  • Lopinavir (LPV) hii ina madhara mwilini kama kuharisha sana, kuharibu kongosho na kusababisha magonjwa yatokanayo na uharibifu wa kongosho na hutolewa kwa tahadhari kwa wenye magonjwa ya ini 

 

MABADILIKO YA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VVU

Kipindi cha nyuma dawa pendekezi  ilikua TLE lakini madhara ya matumizi yake yameonekana kuwa  mengi kuliko faida  zake. Madhara hayo yametokana na uwepo wa dawa ya Efavirenz katika mjumuisho wa dawa ya TLE iliokua ikisababisha  wagonjwa kupata ndoto mbaya usiku, degedege, kuchanganyikiwa, kupata msongo wa mawazo na kushindwa kulala usiku.

Kwa sasa mchanganyiko wa dawa pendekezi unaotumika Tanzania ni TLD ambapo imeonekana kuwa yenye  madhara  machache kuliko dawa nyinginezo. Baadhi ya madhara yanayoeza kutokea ni kama  matatizo ya figo, kichefuchefu, kuhara, kizunguzungu na kupoteza hamu ya usingizi. Mchanganyiko huu wa TLD haushauriki kutumika kama mgonjwa ana shinikizo sugu la moyo lisilotibika, kisukari, matatizo ya mfumo wa mkojo na magonjwa yanaoathiri kazi ya ini.

 

UTOAJI TAARIFA WA MADHARA YATOKANAYO NA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VVU

Madhara ya dawa za kupunguza makali ya VVU yamegawanyika katika makundi mawili ,kundi la kwanza yanapelekea kulazwa hospitali kwa muda mrefu.Hii inaeza sababisha madhara ya kudumu au Watoto kuzaliwa na shida katika ukuaji.Kundi jingine la madhara ya hizi dawa linahitaji mabadiliko ya dawa kutoka kundi moja kwenda jingine.

  • Madhara  ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU yanaeza kutambuliwa na watoa huduma za afya kupitia kuongea na wagonjwa kuhusu madhara wanayoyapata, kufanya uchunguzi yakinifu na kupitia rekodi za wagonjwa.

  • Wagonjwa wana budi kutoa taarifa ya madhara ya dawa hizi kwa waatoa huduma wa afya walio katika vituo vya afya vya  karibu ambapo wamekua wakipata hizo dawa. Kupitia hao watoa huduma wa afya watasaidia kupeleka taarifa kwa Nyanja za juu kitaifa na kusaidia kupunguza madhara yaambatanayo na hizi dawa za VVU.

Leave a comment