Fahamu mambo yanayoweza sababisha upungufu wa mbegu za kiume (sperm count)

Fahamu mambo yanayoweza sababisha upungufu wa mbegu za kiume (sperm count)

Ili kufanikisha kutunga mimba mwanaume anatakiwa azalishe mbegu kuanzia million 20 na zaidi katika kila millilita moja ya shahawa. kuna baadhi hutengeneza kiwango kidogo cha mbegu hizo na hii hutokana na sababu mbalimbali za kiafya,kimazingira na mfumo wa maisha ya kila siku.

 

Sababu Za Kiafya

1. Matumizi ya dawa kwa muda mrefu hususani dawa za kutibu fangasi, na kurekebisha homoni.

2. Mabadiliko ya mfumo na utengenezaji wa homoni mwilini.

3. Kinga za mwili kushambulia mbegu za kiume.

4. Ukosefu wa lishe bora hasa yenye zinc, folic acid, vitamini E, C, na B12.

5. Uzito uliopitiliza (obesity).

Mazingira

1. Mionzi hususani ya x-ray ambayo huharibu mfumo wa utengenezeja wa mbegu.

2. Kukaa kwenye mazingira yenye joto kali kama vile viwandani au jikoni kwa muda mrefu.

3. Kemikali za viwandani kama vile sumu za kuulia wadudu.

4. Kupakata vifaa vya kielekroniki kama vile laptop kwa muda mrefu.

5. Mazingira na aina ya kazi mfano madereva wa safari ndefu.

 

Mfumo wa Maisha

 

1. Matumizi ya sigara na pombe kupita kiasi.

2. Msongo wa mawazo na sonona.

3. Kujichua (masterbation) hupunguza kiasi kikubwa cha mbegu na nguvu za kiume.

4. Aina ya vyakula vinavyoliwa hususani vyakula vyenye mafuta mengi.

5. Kutofanya mazoezi ya viungo. 

 

Tatizo la kupungua kwa mbegu za kiume linazuilika na kutibika pia. Muhimu ni kuzingatia lishe bora na mazoezi pia kujiepesha na mazingira yanayoweza kuwa sababu ya kupunguza uzalishaji wa mbegu. endapo tatizo hilo litaendelea kwa muda mrefu usisite kuonana na madaktari ili kulitatua.


Leave a comment