Fahamu suluhisho la Fangasi sugu za ukeni.

Fahamu suluhisho la Fangasi sugu za ukeni.

Kwa kawaida eneo la uke huwa na kiasi kikubwa cha bakteria (Lactobacillus) ukilinganisha na kiasi cha fangasi. Bakteria hawa wapo kwa ajili ya kudhibiti ukuaji wa fangasi na inapotokea mabadiliko kama matumizi ya antibayotiki kwa kipindi kirefu, kiasi kikubwa cha homoni wakati wa balehe na ujauzito au kushuka kwa kinga ya mwili sababu ya magonjwa kama kisukari au UKIMWI ndipo fangasi hawa hushamiri.


Fangasi aina ya “Candida albicans” ndiyo anayehusishwa zaidi na tatizo hili na huwakumba zaidi wanawake kati ya umri wa miaka 20-40.

Je nitajuaje kama nina fangasi ukeni?

1.Kuwashwa na kupata maumivu ukeni

2.Maumivu kama unaungua na moto wakati wa kukojoa au kufanya mapenzi

3.Kutokwa na uchafu mweupe, mzito, uliogandiana, usio nharufu na unaofanana na jibini (cheese).

“Ni muhimu kumuona daktari uonapo dalili hizi au zaidi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi.

Je Nifanye nini kuepukana na Tatizo Hili?

1.Weka uke wako katika hali ya usafi; tumia sabuni isiyo na madawa makali kujisafisha kwa nje tu na jisuuze kwa maji ya kutosha.

2.Baada ya kujisaidia jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma kuzuia kusambaza vijidududu kutoka njia ya haja kubwa.

3. Vaa nguo za ndani zenye uwezo wa kufyonza unyevu hasa zilizotengenezwa na pamba.

4. Badilisha nguo zako mara tu unapomaliza kuogelea kuepusha unyevu.

5. Zingatia ngono salama kwa kutumia kinga (kondumu).

"Badili pedi yako mara kwa mara unapokua kwenye hedhi"

“TATIZO LA FANGASI HUWAKUMBA WENGI NA HUWA NI KERO ILA HABARI NJEMA NI KWAMBA LINATIBIKA NA KUEPUKIKA”


1 comment

  • conrad

    nice it increase a lot of knowledge


Leave a comment