Huduma ya kangaroo kwa mtoto njiti na umuhimu wake

Huduma ya kangaroo kwa mtoto njiti na umuhimu wake

Huduma ya kangaroo ni nini

  • Kangaroo ni huduma spesheli inayotolewa kwa watoto wachanga waliozaliwa njiti na wenye uzito wa kiwango cha chini kuliko ilivyo kawaida.  Ni huduma inayohusisha kugusisha moja kwa moja ngozi ya kifua cha mama na ngozi ya mtoto.
  • Huduma hii imeanza kutolewa mnamo mwaka 1978 katika nchi ya huko Colombia baada ya kuwa na upungufu wa nyenzo kama incubators zinazosaidia kuwapa joto watoto walio njiti na walio na uzito mdogo. Huduma hii imeonyesha kuwa njia bora na mbadala kwa miaka mingi katika nchi zinazoendelea katika kuhudumia watoto njiti.

Shirika la afya duniani limeonyesha kuwa kati ya vifo milioni nne vinavyotokea kwa watoto wachanga, theluthi tano ya vifo hivyo husababishwa na mtoto kuwa njiti au uzito wa kiwango cha chini. Huduma hii imeonyesha kusaidia kupunguza idadi ya vifo vya watoto hawa.

Huduma hii huanza kutolewa hospitali na huweza kutolewa nyumbani pia.

Huduma hii husaidia kudhibiti kiwango cha joto kinachotakiwa kwa mtoto hasa kwa watoto waliozaliwa na uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya miezi kutimia. Hii ni kwa sababu watoto hawa wapo katika hatari ya kupoteza joto la mwili na huweza pelekea kifo kwa mtoto kwa sababu mwili wake hauwezi kuhimili mabadiliko ya joto na kuliweka sawa

Faida za huduma ya kangaroo

  • Inakuza uhusiano na ukaribu wa mtoto
  • Husaidia uzalishaji wa maziwa kwa wingi kwa mama
  • Hurahisisha kunyonyesha kwa wingi na mara nyingi
  • na hivi huongeza ukaribu wa mama na mtoto, huboresha afya ya mtoto
  • Inaaminika kusaidia kupunguza uwezekano wa mtoto kupata maambukizi ya magonjwa akiwa hospitalini na kupunguza siku za mtoto kukaa hospitalini mara baada ya kuzaliwa.

 

 


Leave a comment