Inawezekana mwanaume kuota matiti?

Inawezekana mwanaume kuota matiti?

NDIO, Mwanaume anauwezo wa kuota matiti nahii hutokana na sababu mbalimbali na kitaalamu huitwa gynecomastia ambayo  humaanisha kukuwa kuliko kawaida yake kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissue , tatizo la kuota matiti kwa wanaume limekuwa kubwa sana katika dunia ya leo na huwapata watoto wachanga na  wanaume walio katika umri wa kubalehe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.

 

NINI HUTOKEA?

Mwili wa binadamu una vichocheo ambavyo husaidia kufanya kazi kwa uwiano, na ikitokea kuharibika kwa namna moja au nyingine kwa uwiano huo hupelekea madhara. Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo ujulikananao kama estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu na hivyo basi kupelekea kukua kwa matiti . Hii ni kawaida kwa wanawake kwani huwa na estrogen nyingi hasa wakati wa kubalee na hii hupelekea kukua kwa matiti. 

 

VITU GANI HUPELEKEA/HUONGEZA UWEZEKANO WA MWANUME KUOTA MATITI?

 • Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.
 • Kuwa na  uzito uliopitiliza (Obesity).
 • Utumiaji wa  pombe kupita kiasi.
 • Magonjwa sugu ya figo au ya Ini.
 • Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.
 • Kutumia dawa za mda mrefu kama za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV)

NINI KIFANYIKE KWA MWANAUME MWENYE TATIZO LA KUOTA MATITI?

Kwanza inabidi mlengwa kwenda hospitali na kuonana na mtaalamu wa afya na kufanyiwa vipimo vya uchunguzi kulingana na maelezo atakayotoa na pia dalili na viashiria vya mgonjwa baada ya kupimwa na daktari.

JE, KUNA TIBA YA TATIZO HILI?

Kuota matiti katika umri mdogo chini ya miaka 18 mara nyingi huisha yenyewe bila tiba lakini ikitokea zaidi ya umri wa miaka 18 basi inawezekana ikawa ni shida hivyo basi kuhitaji kuonana na mtaalamu wa afya ili kupata tiba sahihi.

Tiba hutegemea sababu iliyopelekea kukua kwa matiti, na hivyo basi kuna tiba kwa njia zifuatazo:

 • Tiba ya madawa
 • Tiba ya kutumia vichocheo (Testerone Replacementtherapy).
 • Tiba ya Upasuaji 
 • Kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi na kula mlo kamili
 • Kutibu chanzo au magonjwa mbalimbali kama ugonjwa wa figo , ini au saratani.
 • Kuacha unywaji pombe kupita kiasi.

ANGALIZO

Wanaume wenye tatizo hili wapo kwenye hatari zaidi ya mara tano ya kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na wanaume ambao hawana tatizo hili hivyo basi ni vyema kuonana na daktari ili kufanya uchunguzi mapema na kupata tiba sahihi.

Tatizo hili hupelekea mtu kuona aibu na kuathirika kisaikolojia na huenda kupelekea kuwa na huzuni kwa kuhisi yupo tofauti na wanaume wengine,hasa katika jamii zetu za kiafrika ambapo ni kitu kigeni. 


Leave a comment