Je wajua, ukisukutua baada ya kupiga mswaki unakuwa umefanya kazi bure?.

Je wajua, ukisukutua baada ya kupiga mswaki unakuwa umefanya kazi bure?.

Je wajua?

Watu wengi hawafahamu kuwa kusukutua au kusafisha kinywa na maji baada ya kupiga mswaki ni kama umefanya kazi bure tu. Kupiga mswaki kwa kutumia dawa kuna lengo la kuyapa meno yako kinga dhidi ya kutoboka kutokana na uwepo wa madini ya floridi ndani ya dawa ya meno(toothpaste).

 

Wataalamu wanasemaje?

Kitaalamu inashauriwa kutumia dawa ya meno yenye kiasi cha angalau 1000ppm cha madini ya floridi. Kupiga mswaki ndiyo njia pekee ambayo inafikisha madini haya kwenye meno kirahisi na kwa kiasi kikubwa,hivyo inashauriwa kuacha dawa ya meno mdomoni kwa muda fulani ili kupata ulinzi madhubuti dhini ya kutoboka kwa meno(dental caries).

 

Wengi wanafanyaje?

Ajabu ni kwamba wengi wetu huwa tunatabia ya kusukutua au kuosha kinywa kwa maji kila tunapomaliza kupiga mswaki hii siyo sahihi kwani unaposukutua unaondoa dawa yote na madini yote ya floridi ambayo ulikuwa umeyapata kupitia dawa yako hivo unakuwa umefanya kazi bure kabisa maana kinywa chako kinabakia bila ulinzi wowote na meno yako yanakuwa kwenye hatari ya kutoboka pale utakapotumia vyakula vya sukari.

 

Ushauri

Unashuriwa kupiga mswaki na kutema dawa tu mpka pale ambapo hutokuwa na kitu kingine cha kutema, na sababu dawa zingine zina ladha kali au ya uchungu unashauriwa kutumia mswaki wako kuulowanisha na maji kasha kuupitisha kwenye ulimi tu kuondoa ile ladha na kisha kuendelea na ratiba zako kama kawaida.

 

Jenga leo tabia ya kutumia dawa yako ya meno vizuri usisukutue baada ya kupiga mswaki acha dawa ifanye kazi. Tumia dawa yako vizuri,epuka dawa zisizo na madini ya floridi,onana na daktari wa meno angalau mara mbili kwa mwaka.

 


Leave a comment