Mambo yanayoweza sababisha upungufu wa mbegu za kiume (sperm count)

Mambo yanayoweza sababisha upungufu wa mbegu za kiume (sperm count)

Ili kufanikisha kutunga mimba mwanaume anatakiwa azalishe mbegu kuanzia million 20 na zaidi katika kila millilita moja ya shahawa. Baadhi hutengeneza kiwango kidogo cha mbegu hizo na hii hutokana na sababu mbalimbali za kiafya,kimazingira na mfumo wa maisha ya kila siku.

 

1. Sababu za Kiafya

 

- Matumizi ya dawa kwa muda mrefu hususani dawa za kutibu fangasi, na zakurekebisha homoni

- Mabadiliko ya mfumo na utengenezaji wa homoni mwilini

- Kingamwili kushambulia mbegu 

- Ukosefu wa lishe bora hasa yenye zinc, folic acid, vitamini E, C, na B12

- Uzito uliopitiliza (obesity).

 

2. Mazingira

- Mionzi hususani ya x ray ambayo huharibu mfumo wa utengenezeja wa mbegu

- Mazingira yenye joto kali kama vile viwandani au jikoni kwa muda mrefu

- Kemikali za viwandani kama vile viuajisumu vya wadudu.

- Kupakata vifaa vya kielekroniki kama vile laptop kwa muda mrefu

- Mazingira na aina ya kazi mfano madereva wa safari ndefu.

 

3. Mfumo wa Maisha

- Matumizi ya sigara na pombe kupita kiasi

- Msongo wa mawazo na sonona

- Aina ya vyakula vinavyoliwa hususani vyakula vyenye mafuta mengi

- Kutofanya mazoezi ya viungo. 


Leave a comment