Nataka kupunguza uzito bila kufanya mazoezi, je inawezekana?

Asilimia yetu kubwa tunataka kupungua lakini mazoezi huwa ni kikwazo kwetu kutokana na majukumu tuliyonayo au ukosefu wa msukumo ndani yetu wa kufanya mazoezi.
Zifuatazo ni njia za kupunguza uzito pasipo kufanya mazoezi.
1.Kula chakula chenye protini kwa wingi.
Protini katika mwili hufanya kazi ya kusaidia homoni zinazoshibisha na kukufanya ukinai kwa haraka ,hivyo kupunguza njaa na hukufanya ule chakula kidogo,mfano wa vyakula venye protini ni kama vile mayai,samaki,maziwa,nyama,jamii ya kunde kama vile soya,maharage
2.Kunywa maji mara kwa mara
Haswa kabla ya mlo wako,hii husaidia ule chakula kidogo ,vilevile pendelea kunywa maji yenye uvugu vugu haswa unapoamka asubuhi.Maji ya uvuguvugu huongeza joto mwilini na kuongeza kasi ya kumeng’enya chakula hivyo kupunguza mafuta mwilini,hatimaye na uzito kupungua pia.
3.Hakikisha unatafuna chakula chako vizuri na kwa taratibu.
Ubongo wako unahitaji mda wa kutosha kukubali kwamba ulichokula kinakutosha na hauhitaji nyongeza,hivyo basi itakufanya ule kidogo na utosheke kwa haraka zaidi.
4.Pata usingizi wa kutosha na upunguze msongo wa mawazo.
Inapokuja katika swala la afya ,wengi wetu huwa tunaweka usingizi na msongo wa mawazo pembeni.Hivi viwili vina nguvu kubwa katika hamu ya chakula pamoja na uzito.
Ukosefu wa usingizi pamoja na usongo wa mawazo huingiliana na kazi za homoni zinazokupa hamu ya chakula ,na hivyo basi huongeza hamu ya vyakula visivyo na afya,mbali zaidi hukuhatarisha na magonjwa yasioambukizwa.
5.Achana na vinywaji venye sukari
Ni rahisi sana kuongeza uzito kupitia vinywaji venye sukari kwa maana ni vinywaji vya hamu tu,lakini zina kalori kubwa .
Leave a comment