Njia bora ya kumlaza mwanao (chini ya mwaka mmoja)

Njia bora ya kumlaza mwanao (chini ya mwaka mmoja)

Utangulizi

 • Watoto hasa walio chini ya mwaka mmoja ni kundi lililo katika hatari kubwa sana ya kupata magonjwa hivyo huhitaji uangalizi mkubwa sana kutoka kwa wazazi wao wakati wakiwa macho na wakati wakiwa wamelala
 • Kati ya hatari kubwa wakati wa kulala watoto wanayopata ni kupata tabu ya kupumua, kutapika usiku na kadhalika

Njia hizi ni;

 1. Kulala kwa mgongo
 • Hii ndio njia bora ya kumlaza mtoto kulingana na watafiti wengi wa mambo ya masuala ya usingizi kwa watoto
 • Kwanza hupunguza uwezekano wa mtoto kutapika akiwa usingizini (Gastro-Oesophageal Reflex) kwa sababu huacha njia ya hewa kuwa wazi muda wote wa usingizi
 • Huweza badili umbo la kichwa cha mtoto kwa kuwa hakijakomaa bado hasa upande wa kichogo, hali hii hutengamaa akifikisha mwaka mmoja

 

 1. Kulala kwa tumbo
 • Huweka presha kubwa kwenye taya ya mtoto wakati anapolala
 • Uso wa mtoto upo karibu sana na godoro na kusababisha mzunguko mdogo wa hewa, hivyo mtoto ana hatari kubwa ya kupumua hewa aliyoitoa nje mwenyewe
 • kama usafi sio mzuri, inaweza ikawa njia nzuri ya wadudu kuingia kwa njia ya hewa
 • Ilikuwa ikifahamika kuwa watoto wanalazwa kwa tumbo ili wasiweze kupaliwa na matapishi yao kama wakitapika lakini stadi zinaonesha mtoto mwenye afya hata akilala kwa mgongo anaweza kugeuza kichwa wakati akitapika na kuzuia kupaliwa
 1. Kulala kwa ubavu
 • Sio salama kwani mtoto ana hatari ya kugeuka na kulalia tumbo na kuleta matatizo katika upumuaji na maradhi

Vitu vya kuzingatia sehemu mtoto anapolala

 • Usafi ni jambo la msingi kumuepusha mtoto na maradhi, katika kipindi hiki mtoto anakuwa anapata kinga kutoka kwa maziwa ya mama hivyo unyonyeshaji na usafi ni kati ya vitu muhimu kumlinda mtoto na magonjwa
 • Godoro la kutumika ni vyema likawa gumu kiasi na lisilobonyea sana kuzuia uso wa mtoto kujichimbia kwenye godoro na kumpa shida katika kupumua
 • Ni vyema kufunika kichwa cha mtoto na nguo nyepesi na sio nzito kama zinazotumika kifuani na maeneo mengine ili kuruhusu upumuaji mzuri wa mtoto wakati wa kulala
 • Stadi iliyofanyika mjini Berlin, imeonesha kuwa na kupungua kwa vifo vya watoto wakati wa kulala na upataji wa chanjo ya DPT

Mengineyo

 • Kwa watoto wa miezi mitano na kuendelea imeonekana wana kawaida ya kugeuka na kulalia tumbo hivyo ni kawaida na kwa muda huu wanaonekana kuwa na uwezekano mdogo wa kupatwa na shida wakati wa kulala
 • Matatizo wakati wa kulala kwa watoto hutokea sanasana miezi minne ya kwanza ya maisha lakini huwepo mpaka mwaka mmoja hivyo uangalifu inabidi uwepo kwa muda wote huo
 • Kuegemea tumbo kuna umuhimu wake kwa watoto na inaweza fanywa wakati akiwa macho kumpa mazoezi ya kukomaza tumbo, shingo na hata mgongo wake ambazo kutamjengea nguvu ya kujigeuza ahitajipo kufanya hivyo

Leave a comment