Vipele vitokanavyo na Nepi /Pampers

Vipele vitokanavyo na Nepi /Pampers

Utangulizi

 • Pasipo kuwa na matumizi sahihi ya nepi au pampers, huweza kupelekea mtoto kupata vipele katika maeneo ya nyonga, katikati ya mapaja na hata kwenye makalio.
 • Kwa kuanzia huweza kutokea vipele, inaweza kuwa na muwasho na wekundu sehemu tajwa hapo juu au katika hali mbaya Zaidi inaweza leta majipu ambayo huweza kupasuka na kusababasha maumivu makali kwa mtoto.
 • Kwa kawaida huweza kuisha ndani ya siku 4 mpaka 5 baada ya kuanza matibabu
 • Watoto walio na umri wa miezi 4 mpaka miezi 15 hupatwa na vipele hivi hata kila baada ya miezi miwili

Vyanzo vikuu vinavyosababisha vipele hivi

 • Unyevu uliopita kiasi
 • Msuguano uliopitiliza katikati ya mapaja
 • Kuwepo kwa nepi au pampers ya mtoto yenye mkojo au choo kwa muda mrefu (kushindwa kumbadilisha mtoto nepi kwa muda muafaka)
 • Maambukizi ya bakteria au fangasi
 • Aleji inayotokana na nepi au pampers yenyewe

Vitu vya kuzingatia

 1. Kwanza ni kuhakikisha mwanao anakuwa mkavu na msafi kuepusha vipele hivi
 2. Kubadilisha nepi au pampers ya mtoto mara baada anapojisaidia
 3. Usikaze sana nepi au pampers ya mtoto ili kuachia nafasi hata akijisaidia ngozi yake isishikane sana na choo au mkojo

Nini cha kufanya kama mwanangu ana vipele hivi

 1. Tumia maji na kitambaa chepesi kumsafisha mtoto akiwa amejisaidia, unaweza tumia sabuni kama amepata haja kubwa kumsafisha
 2. Wakati wa kumkausha unashauriwa kufuta kwa kiasi na kuacha akauke kwa upepo
 3. Tumia mafuta kiasi kufanya ngozi iwe laini na kuzuia michubuko katikati ya mapaja
 4. Onana na daktari kupewa dawa za ngozi mara nyingi huwa za kupaka na poda zitakazomfaa mwanao kama bado vipele vipo.

Dalili za hatari

 • Vipele visivyopona siku 4-5 baada ya kuanza matibabu
 • Vipele vimesababisha majipu au usaha
 • Mtoto kuanza kupata homa
 • Maumivu makali akiguswa sehemu hizo

Leave a comment