Visababishi vya kuchelewa au kukosa kupata hedhi

Visababishi vya kuchelewa au kukosa kupata hedhi

Je,Una hofu kwa sababu umechelewa kuona siku zako, na unajua wewe si mjamzito?

Kuchelewa kuona siku zako au kuzikosa hutokea kwa sababu mbalimbali tofauti na ujauzito.

Wanawake wengi huona siku zao baada ya siku 28. Ingawa mzunguko wa hedhi kawaida huweza kutumia siku 21 hadi siku 35. Ikiwa hujapata hedhi katika kipindi hiki, zifuatazo huweza kuwa visababishi:

1. Msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo huweza kubadili homoni zako, kubadilisha ratiba yako ya kila siku, na hata kuathiri sehemu ya ubongo wako unaohusika na kumudu hedhi zako.

Msongo wa mawazo huweza kusababisha ukaugua au uzito kushuka au kupanda, ambayo zote yanaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi

Uzito mdogo au uliokithiri.

2. Uzito kuwa mdogo au kukithiri huweza kuathiri mzunguko wa hedhi

Kuwa na uzito asilimia 10 chini ya uzito wa kawaida kwa urefu wako unaweza kubadilisha njia ya kawaida ya kupata hedhi.

Pia inaweza kusababishwa kutokana na kuwa na uzito mkubwa. Kuwa na uzito wa kawaida hurudisha mzunguko wa hedhi katika hali ya kawaida.

 kujua kama uzito wako ni sahihi ingia hapa:

http://daktarimkononi.com/2018/03/15/je-uzito-wako-ni-salama-kwa-afya-yako/

3. Vidonge vya uzazi wa mpango.

Unaweza kupata mabadiliko katika mzunguko wako wakati unatumia vidonge vya uzazi wa mpango. Vidonge hivi huwa na homoni ya estrogen na progesini, ambayo huzuia mayai yako kutoka. Inaweza kuchukua hadi miezi sita kwa mzunguko wako kurudi katika hali ya kawaida tena baada ya kuacha vidonge hivyo.

Fahamu Zaidi: 
 Inaweza kuchukua hadi miezi sita kwa mzunguko wako kurudi katika 
 hali ya kawaida tena baada ya kuacha vidonge hivyo.

4. Magonjwa ya kudumu & ya muda mrefu.

Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari yanaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi.

Mabadiliko katika sukari katika damu yanauhusiano mkubwa na mabadiliko ya homoni, hivyo kisukari kisichodhibitiwa kinaweza kusababisha hedhi yako kubadilika.

5. Magonjwa ya tezi ya thyroid

Tezi kutokufanya kazi au kufanya kazi sana huathiri mzunguko wa hedhi kwa kiasi kikubwa. Matatizo ya tezi hii huweza kutibiwa kwa dawa na hedhi ikarudi kama kawaida.

 

    1 comment

    • Jack

      Asante sana kwa elimu hii


    Leave a comment